18. AKIFA YESU NIKAFA NAYE

AKIFA YESU NIKAFA NAYE

1.  Akifa Yesu nikafa naye,
Uzima upya huishi naye;
Humtazama mpaka aje
Nyakati zote ni wake Yeye.

Chorus:
Nyakati zote nimo pendoni,
Nyakati zote ni uzimani,
Humtazama hata atokee,
Nyakati zote mimi ni wake.
 
2.  Vita sipigi visivyo haki,
Na Bwana wangu hapiganiki;
Beramu yake haitwaliki,
Napo po pote hila sitaki.
 
3.  Sina mashaka, akawa mbali;
Mizigo yote aihimili;
Ananituliza Imanweli,
Nyakati zote mimi husali.
 
4.  Sina huzuni na mimi sidhii;
Simwagi chozi, wala siguni;
Sikuti afa, ila Kitini
Daima hunifikiri mimi.
 
5.  Kila unyonge huusikia;
Kila ugonjwa kwake hupoa;
Yesu ni mwenye kuniokoa
Nyakati zote hunijalia.

Comments