Posts

Showing posts from March, 2022

12. EWE ROHO WA MBINGUNI

EWE ROHO WA MBINGUNI 1.    Ewe Roho wa Mbinguni Uje kwetu sasa. Ufanye makazi yako Ndani ya kanisa.   2.    Ndiwe mwanga, umulike Tupate jikana; Mengi kwetu yapunguka, Tujalize, Bwana.   3.    Ndiwe Moto, teketeza Taka zetu zote: Moyo na iwe sadaka Ya Mwokozi, yote.   4.    Ndiwe umande, na kwako Tutaburudika, Nchi kavu itakuwa Ni yenye baraka.   5.    Roho wa Mbinguni uwe Nasi hapa chini, Mwili uufananishe Na Kichwa Mbinguni.

13. TAFUTA DAIMA UTAKATIFU

TAFUTA DAIMA UTAKATIFU 1.    Tafuta daima utakatifu; Fanya urafiki na Wakristo tu; Nena siku zote na Bwana wako, Baraka uombe kwa kila jambo.   2.    Tafuta daima utakatifu; Uwe peke yako ukimwabudu; Ukimwangalia mwokozi wako, Utabadilishwa kama alivyo.   3.    Tafuta daima utakatifu; Kiongozi wako awe Yesu tu; Katika furaha au huzuni Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.   4.    Tafuta daima utakatifu; Umtawaze Roho moyoni mwako; Akikuongoza katika haki, Hufanywa tayari kwa kazi yake.

14. YESU KWA IMANI

YESU KWA IMANI 1.    Yesu kwa imani, Nakutumaini, Peke yako; Nisikie sasa, Na kunitakasa, Ni wako kabisa Tangu leo.   2.    Nipe nguvu pia Za kusaidia Moyo wangu; Ulikufa Wewe, Wokovu nipewe Nakupenda Wewe, Bwana wangu.   3.    Hapa nazunguka Katika mashaka, Na matata; Palipo na giza Utaniongoza Hivi nitaweza Kufuata.   4.    Takuwa mzima Nivushe salama Mautini; Sina hofu kamwe Ukiwapo nami Nami nikwandame Siku zote.

15. CHA KUTUMAINI SINA

CHA KUTUMAINI SINA 1.    Cha kutumaini sina Ila damu yake Bwana, Sina wema wa kutosha Dhambi zangu kuziosha.   Chorus: Kwake Yesu nasimma, Ndiye Mwamba: ni salama Ndiye mwamba: ni salama.   2.    Njia yangu iwe ndefu Yeye hunipa wokovu; Mawimbi yakinipiga Nguvu zake ndiyo nanga.   3.    Damu yake na sadaka Nategemea daima, Yote chini yakiisha Mwokozi atanitosha.   4.    Nikiitwa hukumuni, Rohoni nina amani; Nikivikwa haki yake Sina hofu mbele zake.

16. KUMTEGEMEA MWOKOZI

KUMTEGEMEA MWOKOZI 1.     Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa; Kukubali neno lake Nina raha moyoni. Chorus: Yesu,Yesu namwamini, Nimemwona thabiti; Yesu,Yesu, yu thamani, Ahadi zake kweli.   2.    Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa, Kuamini damu yake Nimeoshwa kamili.   3.    Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa, Kwake daima napata Uzima na amani.   4.    Nafurahi kwa sababu Nimekutegemea; Yesu, Mpendwa na Rafiki Uwe nami dawamu.

17. NAMWADAMA BWANA

NAMWADAMA BWANA 1.    Namwadama Bwana kwa alilonena Njia yangu huning’azia; Nikimridhisha atanidumisha Taamini nitii pia.   Chorus: Amini utii, njia pweke ni hii Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii.   2.    Giza sina kwangu wala hata wingu Yeye mara huviondoa Woga, wasiwasi, sononeko, basi; Huamini nitii pia.   3.    Masumbuko yote, sikitiko lote; Kwa mapenzi hunilipia; Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki, Taamini nitii pia.   4.    Mimi sitajua raha sawasawa Ila yote Yesu kumpa; Napata fadhili na radhi kamili, Taamini nitii pia.   5.    Nitamfurahia na kumtumaini, Majumbani na njia-njia; Agizo natenda; nikitumwa hwenda, Huamini nitii pia.

18. AKIFA YESU NIKAFA NAYE

AKIFA YESU NIKAFA NAYE 1.    Akifa Yesu nikafa naye, Uzima upya huishi naye; Humtazama mpaka aje Nyakati zote ni wake Yeye. Chorus: Nyakati zote nimo pendoni, Nyakati zote ni uzimani, Humtazama hata atokee, Nyakati zote mimi ni wake.   2.    Vita sipigi visivyo haki, Na Bwana wangu hapiganiki; Beramu yake haitwaliki, Napo po pote hila sitaki.   3.    Sina mashaka, akawa mbali; Mizigo yote aihimili; Ananituliza Imanweli, Nyakati zote mimi husali.   4.    Sina huzuni na mimi sidhii; Simwagi chozi, wala siguni; Sikuti afa, ila Kitini Daima hunifikiri mimi.   5.    Kila unyonge huusikia; Kila ugonjwa kwake hupoa; Yesu ni mwenye kuniokoa Nyakati zote hunijalia.

19. NDIYO DHAMANA, YESU WANGU

NDIYO DHAMANA, YESU WANGU 1.    Ndiyo dhamana, Yesu wangu; Hunipa furaha za Mbingu; Mrithi wa wokovu wake Nimezawa kwa Roho yake. Chorus: Habari njema, raha yangu Yesu ndiye Mwokozi wangu, Habari njema, raha yangu Yesu ndiye Mwokozi wangu.   2.    Kumsalimu moyo wangu, Mara namwona raha yangu; Aniletea malaika, Wananilinda, taokoka.   3.    Sina kinyume; nashukuru, Mchana kutwa huja kwangu; Usiku kucha kuna nuru; Mwokozi wangu; ndimi huru.   4.    Hali na mali anitwaa! Mara namwona anifaa, Nami nangoja kwa subira; Akiniita, nije mara.

20. NINAYE RAFIKI NAYE

NINAYE RAFIKI NAYE 1.    Ninaye Rafiki naye Alinipenda mbele; Kwa kamba za pendo zake Nimefungwa milele; Aukaza moyo wangu, Uache mageule, Mimi wake, Yeye wangu Ndimi naye milele.   2.    Ninaye rafiki ndiye Aliyenifilia; Alimwaga damu yake Kwa watu wote pia; Sina kitu mimi pia, Nikiwa navyo tele; Pia vyote ni amana Ndimi wake milele.   3.    Ninaye Rafiki naye Uwezo amepewa; Atanilinda mwenyewe, Juu tachukuliwa; Nikitazama Mbinguni, Hupata nguvu tele; Sasa natumika chini, Kisha juu milele.   4.    Ninaye Rafiki naye, Anao moyo mwema; Ni mwalimu, kiongozi, Mlinzi wa daima; Ni nani wa kunitenga Na Mpenzi wa mbele? Kwake nimetia nanga, Ndimi wake milele.

21. ROHO YANGU HIMA

ROHO YANGU HIMA 1.    Roho yangu hima, na taa yako Kaiwashe vyema, hapa si pako; Nguvu zote pia za duniani Hazitakudhuru ukiamini. Chorus: Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma, Yesu vivyo kando, walindwa vyema.   2.    Adui shetani, na nguvu zake, Bwana ameshinda, kwa kifo chake; Wewe nguvu huna, huna kabisa, Ndiwe mpungufu, mnyonge hasa.   3.    Toka na mapema, mbele ya wote, Omba, bisha sana, maisha yote; Vita vikaliko, macho ukae, Jivike silaha, nawe sishindwe.   4.    Bwana Yesu ndiye kwako Mchunga, Neno lake Bwana ndilo upanga; Mbingu zitakwisha, na nchi pia, Neno lake Bwana laendelea.

22. KALE NILITEMBEA

KALE NILITEMBEA 1.    Kale nilitembea Nikilemewa dhambi Nilikosa Msaada, Kuniponya mateso. Chorus: Usifiwe Msalaba! Lisifiwe kaburi! Linalozidi yote, Asifiwe Mwokozi!   2.    Hata nilipofika, Mahali pa Msalaba, Palinifaa sana, Sitasahau kamwe.   3.    Hicho ndicho chanzo Cha kufurahi kwangu. Hapo ndipo mzigo, Uliponituliwa.   4.    Panapo Msalaba, Kinatolewa cheti, Cha kuingia Mbinguni, Kisicho cha kanisa.   5.    Yule Bwana mjinga, Likwenda bila cheti, Kitumai kwingia, Kama walio nacho.   6.    Lipofika langoni, Akaulizwa cheti Cha kumwonyesha Bwana, Akakutwa hanacho.   7.    Lituhuzunishalo, Ni ninyi msio nacho, Kuwa kama mjinga, Kwa siku ya arusi!   8.    Ubavuni mwa Yesu, Mlitokea damu, Chemchemi ya uzima, Itakasayo roho.   9.    Jitahidi wingie, Damuni mwa Mwokozi, Utafutiwa dhambi, Toka rohoni mwako.

23. NI SALAMA ROHONI MWANGU

NI SALAMA ROHONI MWANGU 1.    Nionapo amani kama shwari, Ama nionapo shida, Kwa mambo yote umenijulisha Ni salama rohoni mwangu.   Chorus: Salama rohoni, Ni salama rohoni mwangu.   2.    Ingawa Shetani atanitesa, Nitajipa moyo kwani Kristo ameona unyonge wangu, Amekufa kwa roho yangu.   3.    Dhambi zangu zote, wala si nusu, Zimewekwa msalabani; Wala sichukui laana yake, Ni salama rohoni mwangu.   4.    Ee Bwana himiza siku ya kuja, Panda itakapolia; Utakaposhuka sitaogopa Ni salama rohoni mwangu.

24. MWOKOZI MOYONI MWANGU

MWOKOZI MOYONI MWANGU 1.    Tangu siku hiyo aliponijia, Akae moyoni mwangu, Sina giza tena, ila mwanga pia Kwa Yesu mwokozi wangu. Chorus: Amani moyoni mwangu, Kwake Yesu, Mwokozi wangu; Sina shaka kamwe, Kwa sababu Yeye, Yu nami moyoni mwangu.   2.    Sina haja tena ya kutanga-tanga, Ndiye kiongozi wangu. Dhambi zangu zote zimeondolewa Na Yesu, Mwanawe Mungu.   3.    Matumaini yangu ni ya hakika, Katika Mwokozi wangu. Hofu zangu na hamu zimeondoka. Kwa kuwa ninaye Yesu.   4.    Siogopi tena nikiitwa kufa, Yu nami daima, Yesu. Mlango wa Mbinguni ni Yeye pia, “Talipa humo kwa damu.”   5.    Nitaketi na yeye huko milele, Nisifu Mwokozi wangu. Nina raha moyoni majira yote, Kwa Yesu, Mwanawe Mungu.

25. NIMEKOMBOLEWA NA YESU

NIMEKOMBOLEWA NA YESU 1.    Nimekombolewa na Yesu Aliyenirehemia; Kwa bei ya mauti yake Nimekuwa mtoto wake.   Chorus: Kombolewa! Nakombolewa na damu; Kombolewa! Mimi mwana wake kweli.   2.    Kukombolewa nafurahi, Kupita lugha kutamka; Kulionyesha pendo lake, Nimekuwa mtoto wake.   3.    Nitamwona uzuri wake, Mfalme wangu wa ajabu, Na sasa najifurahisha, Katika neema yake.   4.    Najua taji imewekwa Mbinguni tayari kwangu; Muda kitambo atakuja, Ili alipo, niwepo.

26. YESU UNIPENDAYE

YESU UNIPENDAYE 1.    Yesu unipendaye Kwako nakimbilia, Ni Wewe utoshaye Mwovu akinijia; Yafiche ubavuni Mwako maisha yangu; Nifikishe Mbinguni Wokoe moyo wangu.   2.    Ngome nyingine sina; Nategemea kwako. Usinitupe Bwana, Nipe neema yako, Ninakuaminia Mwenye kuniwezesha; Shari wanikingia, Vitani wanitosha.   3.    Nakutaka Mpaji Vyote napata kwako; Niwapo muhitaji, Utanijazi vyako; Nao waangukao Wanyonge wape nguvu Poza wauguao, Uongoze vipofu.   4.    Bwana umeniosha Moyo kwa damu yako, Neema ya kutosha Yapatikana kwako; Kwako Bwana naona Kisima cha uzima, Mwangu moyoni, Bwana, Bubujika daima.

27. MUNGU NI PENDO

MUNGU NI PENDO 1.    Mungu ni pendo, apenda watu; Mungu ni pendo, anipenda   Chorus: Sikilizeni furaha yangu, Mungu ni pendo, anipenda.   2.    Nilipotea katika dhambi, Nikawa mtumwa wa Shetani.   3.    Akaja Yesu kunikomboa, Yeye kanipa kuwa huru.   4.    Sababu hii namtumikia, Namsifu yeye siku zote.

28. ANIPENDA NI KWELI

ANIPENDA NI KWELI 1.    Anipenda ni kweli; Mungu anena hili; Sisi wake watoto; Kutulinda si zito. Chorus: Yesu anipenda, Yesu anipenda, Kweli anipenda, Mungu amesema.   2.    Kwa kupenda akafa Niokoke na kufa; Atazisafi taka, Sana ataniweka.   3.    Anipenda kabisa; Niuguapo sasa Anitunza Mbinguni Niliyelala chini.   4.    Kunipenda haachi, Tu sote hapa chini Baada ya mashaka Kwake tanipeleka.

29. BABA YETU ALIYE MBINGUNI

BABA YETU ALIYE MBINGUNI 1.    Baba Yetu aliye Mbinguni Amenifurahisha yakini Kuniambia mwake Chuoni Ya kuwa nami Yesu pendoni.   Chorus: Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda, anipenda; Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda mimi.   2.    Nimuachapo kutanga mbali, Yeye yu vivyo, hupenda kweli. Hunirejeza kwake moyoni; Kweli yu nami Yesu pendoni.   3.    Anipenda! Nami nampenda; Kwa wokovu alionitenda; Akanifia Msalabani Kwa kuwa nami Yesu pendoni.   4.    Haya kujua yanipa raha; Kumuamini kuna furaha; Humfukuza mara Shetani, Kwona yu nami Yesu pendoni.   5.    Sifa ni nyingi asifiwazo, Moja ni sana katika hizo, Wala siachi, hata Mbinguni, Kwimba, “Yu nami Yesu pendoni”.

30. NILIKUWA KONDOO ALIYEPOTEA

NILIKUWA KONDOO ALIYEPOTEA 1.    Nilikuwa kondoo aliyepotea, Sikupenda zizi kamwe, ila kutembea Nilikuwa mwana asiyesikia, Sikupenda Baba yangu wala kutulia.   2.    Na Mchunga mwema alinitafuta, Baba kwa mapenzi ndiye aliyenivuta; Karibu ya kufa, kwa kiu na kwa njaa, Waliniona mnyonge, waliniokoa.   3.    Yesu ni mchunga, mwenziwe hapana, Aliosha taka zangu, dhambi nyingi sana; Kwa vidonda vyangu alitia dawa. Ndiye aliyenipata, na kwake nalindwa.   4.    Nilikuwa kondoo aliyepotea Sasa nampenda Baba, na mchunga pia; Kwanza nilitanga na kukosa sana, Hivi nyumbani mwa Baba sipotei tena.

31. MSINGI IMARA

MSINGI IMARA 1.    Msingi imara, enyi wa kweli, Umekwisha pigwa kwa neno hili, Aongeze lipi? Mnayo pia Kwa Yesu mliomkimbilia.   2.    Wambiwapo vuka maji ya giza, Mito ya mashaka taipunguza; Takuwapo nawe, nikuwezeshe, Ipate kufaa, isikutishe!   3.    Utakapopishwa ndani ya moto Nguvu nitakupa, upate pato; Huteketezwi, ila taka zako, Na zitasalia dhahabu zako.   4.    Hata zije mvi, walio wangu Hawaoni kwisha mapenzi yangu; Nazo zitakapowenea, ndipo Mabegani mwangu niwatwekapo.   5.    Na mtu aliyenitegemea Kamwe kwa adui sitamtia; Nguvu za jehanum zijapotisha, Mtu wangu kamwe sitamuacha.

32. YESU AWAKUBALI WAKOSA

YESU AWAKUBALI WAKOSA 1.    Yesu awakubali, Wakosa, wahalifu, Wambieni wa mbali Habari ya wokovu. Chorus:   Tangazeni kwa bidii, “Akubali wakosa!” Liwe neno dhahiri, “Akubali wakosa!”   2.    Awakubali Bwana Neno lake amini Watu kila aina Waje kwake tengoni.   3.    Mimi ni safi moyo Na mbele ya sharia, Aliye safi roho Kwake ilitimia.   4.    Akubali wakosa; Nami anikubali; Alivyonitakasa Mbinguni niwasili.

33. DHAMBI IKIKULEMEA

DHAMBI IKIKULEMEA 1.    Dhambi ikikulemea, Kwa Bwana rehema; Hivi sasa tegemea Neno la salama.   Chorus: Tegemea, tegemea, akwita sasa. Ni Mwokozi, ni Mwokozi; amini sasa.   2.    Yesu amemwaga damu Ya nyingi baraka; Nawe sasa oga mumu Zioshwamo taka.   3.    Ni njia Yeye hakika Hwongiza rahani; Usikawe kumshika, Uwe barakani.   4.    Karibu nawe wingie Mwetu safarini, Twende tukamwamkie, Milele Mbinguni.

34. NJONI WENYE DHAMBI

NJONI WENYE DHAMBI 1.    Njoni! njoni! Wenye dhambi, Njoni, msikawie; Yesu anawangojea  Ndiye awapendaye; Ajuaye awezaye Kuwaponya ni Yeye.   2.    Ewe muhitaji uje; Anakukaribisha, Imani, kweli, na toba, Neema ya kutosha, Jua sana, kwake Bwana Bure utayapata.   3.    Njoni, mliolemewa Na dhambi ya Adamu; Mkingoja kujiponya Mtapotea mumu; Si wa haki, ni wakosa Waoshwao kwa damu.   4.    Ikamtokea dhiki, Mle Gethisemani; Kisha alipoangikwa Akalia mtini; ” Imekwisha”, alitosha Dhabihu ya thamani.   5.    Kristo aliye Mbinguni Hutuombea huko; Basi mtumai Yeye; Kamwe mwingine hako Yesu pweke, Yesu pweke, Ndiye Mwokozi wako.   6.    Wamsifu-sifu sana Mbinguni malaika, Wachanganya nyimbo zao Na waliookoka: Aleluya wataimba Waliooshwa taka.

35. TWENDE KWAKE

TWENDE KWAKE 1.    Twende kwake, twende kwake, kwake Yesu sasa, Sasa twende kwake, kwake Yesu sasa!   2.    Akwokoe, akwokoe, Bwana Yesu sasa! Sasa akwokoe, Bwana Yesu, sasa!   3.    Msadiki, msadiki, Bwana Yesu sasa, Sasa msadiki, Bwana Yesu sasa!   4.    Anaweza, anaweza, Bwana Yesu sasa, Sasa anaweza, Bwana Yesu sasa!   5.    Anapenda, anapenda, Bwana Yesu sasa, Sasa anapenda, Bwana Yesu sasa!   6.    Njoo hima, njoo hima, kwake Yesu sasa, Sasa njoo hima, kwake Yesu sasa!

36. ANISIKIAYE ALIYE YOTE

ANISIKIAYE ALIYE YOTE 1.    Anisikiaye, aliye yote; Sasa litangae, wajue wote, Duniani kote neno wapate, Atakaye na aje! Chorus: Ni “Atakaye,” ni “atakaye,” Pwani hata bara, na litangae; Ni Baba Mpenzi alinganaye Atakaye na aje.   2.    Anijiliaye, Yesu asema, Asikawe, aje hima mapema; Ndimi njia, Kweli, ndimi Uzima;   3.    Atakaye aje, ndiyo ahadi; Atakaye hiyo, haitarudi! Atakaye lake, ni la abadi! Atakaye na aje.