34. NJONI WENYE DHAMBI
NJONI WENYE DHAMBI
1. Njoni! njoni! Wenye dhambi,
Njoni, msikawie;
Yesu anawangojea
Ndiye awapendaye;
Ajuaye awezaye
Kuwaponya ni Yeye.
2. Ewe muhitaji uje;
Anakukaribisha,
Imani, kweli, na toba,
Neema ya kutosha,
Jua sana, kwake Bwana
Bure utayapata.
3. Njoni, mliolemewa
Na dhambi ya Adamu;
Mkingoja kujiponya
Mtapotea mumu;
Si wa haki, ni wakosa
Waoshwao kwa damu.
4. Ikamtokea dhiki,
Mle Gethisemani;
Kisha alipoangikwa
Akalia mtini;
” Imekwisha”, alitosha
Dhabihu ya thamani.
5. Kristo aliye Mbinguni
Hutuombea huko;
Basi mtumai Yeye;
Kamwe mwingine hako
Yesu pweke, Yesu pweke,
Ndiye Mwokozi wako.
6. Wamsifu-sifu sana
Mbinguni malaika,
Wachanganya nyimbo zao
Na waliookoka:
Aleluya wataimba
Waliooshwa taka.
Comments
Post a Comment