15. CHA KUTUMAINI SINA

CHA KUTUMAINI SINA

1.  Cha kutumaini sina
Ila damu yake Bwana,
Sina wema wa kutosha
Dhambi zangu kuziosha.
 
Chorus:
Kwake Yesu nasimma,
Ndiye Mwamba: ni salama
Ndiye mwamba: ni salama.
 
2.  Njia yangu iwe ndefu
Yeye hunipa wokovu;
Mawimbi yakinipiga
Nguvu zake ndiyo nanga.
 
3.  Damu yake na sadaka
Nategemea daima,
Yote chini yakiisha
Mwokozi atanitosha.
 
4.  Nikiitwa hukumuni,
Rohoni nina amani;
Nikivikwa haki yake
Sina hofu mbele zake.

Comments

Popular posts from this blog

18. AKIFA YESU NIKAFA NAYE