26. YESU UNIPENDAYE

YESU UNIPENDAYE

1.  Yesu unipendaye
Kwako nakimbilia,
Ni Wewe utoshaye
Mwovu akinijia;
Yafiche ubavuni
Mwako maisha yangu;
Nifikishe Mbinguni
Wokoe moyo wangu.
 
2.  Ngome nyingine sina;
Nategemea kwako.
Usinitupe Bwana,
Nipe neema yako,
Ninakuaminia
Mwenye kuniwezesha;
Shari wanikingia,
Vitani wanitosha.
 
3.  Nakutaka Mpaji
Vyote napata kwako;
Niwapo muhitaji,
Utanijazi vyako;
Nao waangukao
Wanyonge wape nguvu
Poza wauguao,
Uongoze vipofu.
 
4.  Bwana umeniosha
Moyo kwa damu yako,
Neema ya kutosha
Yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona
Kisima cha uzima,
Mwangu moyoni, Bwana,
Bubujika daima.

Comments

Popular posts from this blog

18. AKIFA YESU NIKAFA NAYE