24. MWOKOZI MOYONI MWANGU

MWOKOZI MOYONI MWANGU

1.  Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu,
Sina giza tena, ila mwanga pia
Kwa Yesu mwokozi wangu.

Chorus:
Amani moyoni mwangu,
Kwake Yesu, Mwokozi wangu;
Sina shaka kamwe,
Kwa sababu Yeye,
Yu nami moyoni mwangu.
 
2.  Sina haja tena ya kutanga-tanga,
Ndiye kiongozi wangu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa
Na Yesu, Mwanawe Mungu.
 
3.  Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka.
Kwa kuwa ninaye Yesu.
 
4.  Siogopi tena nikiitwa kufa,
Yu nami daima, Yesu.
Mlango wa Mbinguni ni Yeye pia,
“Talipa humo kwa damu.”
 
5.  Nitaketi na yeye huko milele,
Nisifu Mwokozi wangu.
Nina raha moyoni majira yote,
Kwa Yesu, Mwanawe Mungu.

Comments

Popular posts from this blog

18. AKIFA YESU NIKAFA NAYE