14. YESU KWA IMANI

YESU KWA IMANI

1.  Yesu kwa imani,
Nakutumaini,
Peke yako;
Nisikie sasa,
Na kunitakasa,
Ni wako kabisa
Tangu leo.
 
2.  Nipe nguvu pia
Za kusaidia
Moyo wangu;
Ulikufa Wewe,
Wokovu nipewe
Nakupenda Wewe,
Bwana wangu.
 
3.  Hapa nazunguka
Katika mashaka,
Na matata;
Palipo na giza
Utaniongoza
Hivi nitaweza
Kufuata.
 
4.  Takuwa mzima
Nivushe salama
Mautini;
Sina hofu kamwe
Ukiwapo nami
Nami nikwandame
Siku zote.

Comments

Popular posts from this blog

18. AKIFA YESU NIKAFA NAYE