31. MSINGI IMARA

MSINGI IMARA

1.  Msingi imara, enyi wa kweli,
Umekwisha pigwa kwa neno hili,
Aongeze lipi? Mnayo pia
Kwa Yesu mliomkimbilia.
 
2.  Wambiwapo vuka maji ya giza,
Mito ya mashaka taipunguza;
Takuwapo nawe, nikuwezeshe,
Ipate kufaa, isikutishe!
 
3.  Utakapopishwa ndani ya moto
Nguvu nitakupa, upate pato;
Huteketezwi, ila taka zako,
Na zitasalia dhahabu zako.
 
4.  Hata zije mvi, walio wangu
Hawaoni kwisha mapenzi yangu;
Nazo zitakapowenea, ndipo
Mabegani mwangu niwatwekapo.
 
5.  Na mtu aliyenitegemea
Kamwe kwa adui sitamtia;
Nguvu za jehanum zijapotisha,
Mtu wangu kamwe sitamuacha.

Comments

Popular posts from this blog

18. AKIFA YESU NIKAFA NAYE