23. NI SALAMA ROHONI MWANGU

NI SALAMA ROHONI MWANGU

1.  Nionapo amani kama shwari,
Ama nionapo shida,
Kwa mambo yote umenijulisha
Ni salama rohoni mwangu.
 
Chorus:
Salama rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.
 
2.  Ingawa Shetani atanitesa,
Nitajipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu,
Amekufa kwa roho yangu.
 
3.  Dhambi zangu zote, wala si nusu,
Zimewekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake,
Ni salama rohoni mwangu.
 
4.  Ee Bwana himiza siku ya kuja,
Panda itakapolia;
Utakaposhuka sitaogopa
Ni salama rohoni mwangu.

Comments

Popular posts from this blog

18. AKIFA YESU NIKAFA NAYE